Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuimarisha ubora wa elimu katika ngazi zote .

Waziri Ndalichako amesema hayo alipokuwa akizindua Jengo Jipya la Hosteli ya Wanafunzi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kigamboni.

Profesa Ndalichako amesema kuwa pamoja na kujikita kwenye kujenga maadili na uzalendo katika chuo hicho pia amewaagiza kuwa wanahakikisha wanaandaa wanafunzi mahiri na wenye ujuzi utakaowawezesha kuchangia katika uchumi wetu.

“ Ubora wa elimu inayotolewa na Chuo chenu uwe ni wa kiwango cha juu kinachokubalika kitaifa na kimataifa. Na kwa kufanya hivyo mtakuwa pia mmetekeleza Dira yenu ya Elimu ambayo kama Taifa tunataka kuwa na Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katika maendeleo ya Taifa”Amesema Ndalichako.

Waziri Ndalichako amesema Mafanikio ya chuo pamoja na ujenzi wa hostel hiyo ya wanafunzi kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Chuo ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya chuo na pia ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi na Ilani ya uchaguzi ya chama Tawala cha Mapinduzi. 

Aidha alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk .John Pombe Magufuli kwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Ilani ya CCM,  hivyo kuendelea kujenga imani kwa Watanzania ambao ndiyo waliyompa ridhaa kuongoza nchi yetu. 

“Leo hii tunashuhudia uzinduzi wa Hostel hii ambayo ilianza kujengwa Aprili 2012 na ilipaswa kukamilika Januari 2014. Hata hivyo, ujenzi huo ulikuwa umesimama kutokana na ukosefu wa fedha. 

 Tunamshukuru sana Rais ambaye alitembelea Chuo hiki mwezi Agosti 2017 na kuahidi kuwa atahakikisha Shilingi 1,189,000,000 zilizokuwa zinahitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo hili zinapatikana. Kama ilivyo kawaida yake, Mheshimiwa Rais akiahidi anatekeleza, fedha zilipatikana na ujenzi uliokuwa umesimama tangu mwaka 2014 sasa umekamilika na tuko hapa kwa kuzinduzi rasmi wa jengo hilo. 

 Mheshimiwa Rais alipenda sana aje mwenyewe kuzindua, lakini kutokana na majukumu mengi aliyonayo amenituma nifanye kazi hii. Anawapongeza sana kwa kusimamia vizuri kazi hii” Amesema Waziri Ndalichako.

Kwa Upande wake Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila amesema Hostel hiyo mpya itasaidia kupunguza tatizo la malazi, hivyo kuwapa wanachuo mahali pazuri na salama pa kuishi na kuwaongezea muda wa kujisomea. 

Amesema kuwa Hoteli hiyo ambayo inachukua wanafunzi Zaidi ya 700 itaweza kukamilisha idadi ya wanafunzi watakaokuwa wanalala shuleni hapo kuwa Zaidi ya 1000 Hivyo, ni muhimu itunzwe vizuri ili iendelee kuwanufaisha wanafunzi wengi zaidi kwa miaka ijayo.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na Wanafunzi na wagaeni waalikwa waliofika kwenye uzinduzi wa jengo jipya la chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam
MKuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ,Profesa Shadrack Mwakalila akizungumza juu ya historia ya ujezni wa Hosteli hizo. 
Kaimu Mwenyekiti wa bodi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Mashavu Ahmad Fakhi akizungumza kwa Niaba ya Mwenyekiti wa bodi ya Chuo Hicho ,Profesa Mark Mwandosya. 
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako kushoto ni Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Profesa Shadrack Mwakalila na Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa bodi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Mashavu Ahmad Fakhi wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la hosteli ya Wanafunzi
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akipeana mkono wa pongezi na Kaimu Mwenyekiti wa bodi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Mashavu Ahmad Fakhi mara baada ya kuzindua jiwe la Msingi
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akikata utepe kabla ya kuingia kukagua jengo jipya la Hosteli ya Wanafunzi.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akiwa ndani akikagua kwa makini Vitanda na thamani zilizopo ndani ya Hosteli hizo.
Sehemu ya Jengo Jipya la Hosteli ya Wanafunzi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Likionekana kwa nje mara baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa bodi wa chuo hicho
Share To:

Post A Comment: