Monday, 6 August 2018

Safari za nje ya nchi za Kajala zazua gumzoSAFARI za nje ya nchi za muigizaji wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja zimeibua maswali lukuki huku kila mmoja akisema lake.

Siku za hivi karibuni, Kajala amekuwa akisafiri mara kwa mara kuelekea nchini Dubai hali ambayo imewafanya marafiki zake wahoji anapata wapi jeuri ya pesa wakati kazi yake wanaifahamu.

“Kwa kweli tunashindwa kumuelewa mwenzetu hizi safari zake za kila mara Dubai, anapata wapi hii hela maana kama ni kazi za filamu tunajua sasa hivi soko lilivyo gumu,” alihoji rafiki huyo aliyeomba hifadhi ya jina.

Rafiki huyo alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa, mbali na safari hizo, Kajala anatanua sana mjini na inasemekana anashusha bonge la mjengo.

“Kwa kweli mwenzetu sijui ni bwana mpya, sijui ana biashara gani inayomuingizia kipato,” aliongeza rafiki huyo.

Baada ya Ijumaa Wikienda kupata ‘dauti’ hizo kutoka kwa rafiki yake Kajala, lilimtafuta mrembo huyo ambapo alifunguka kuwa kinachompa jeuri ni ubalozi pamoja na kazi yake ya sanaa.

“Wewe unajua mimi ni balozi, pia filamu sijaacha kuigiza iwe ni za watu au za kwangu, mtu anaanzaje kuhoji safari zangu za nje ya nchi?

“Niwashauri wanaoibua hayo maswali kwangu wachape kazi, waache majungu,” alisema Kajala.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: