Saturday, 4 August 2018

Rais Magufuli ampokea Kigwangala afikishwa Muhimbili


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempokea Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amewasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.

Rais Magufuli ameshirikiana na  Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere kumshusha kutoka kwenye ndege Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara.

Ndege hiyo iliwasili majira ya 12 jioni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: