Friday, 31 August 2018

Polisi Kinondoni Yawashikilia mgambo watatu kwa kumshambulia na kumjeruhi Mfanyabiashara

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni linawashikilia mgambo watatu wa manispaa ya Kinondoni kwa tuhuma za kumjeruhi mfanyabiashara, Robson Orotho mkazi wa Bunju jijini Dar es salaam  leo Ijumaa Agosti 31, 2018.

Inaelezwa kuwa mgambo hao walimshushia kipigo mfanyabiashara huyo kutokana na kushindwa kulipa Sh50,000 ya taka.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Jumanne Murilo amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kutokana na kusambaa kwa taarifa zikiwaonyesha wakikiuka sheria za nchi.


"Ni kweli tunawashikilia watuhumiwa watatu kwa kitendo walichokifanya, tumegundua ziko taratibu na sheria zilizokiukwa,watuhumiwa ni Kelvin Edson, Gudluck Festo na Rehema Nyange ambao wote ni mgambo wa manispaa ya Kinondoni"alisema Muliro.

Advertisement
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: