Mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru, Constantine Mathias, amehojiwa na polisi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mitandao na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Akizungumza jana Agosti 23 Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu, Deusdedit Nsimeki alisema Mathias alikamatwa, akahojiwa kisha akaachiwa.

Imeelezwa kuwa Mathias alisambaza picha kwenye mtandao wa kijamii wa facebook inayomuonyesha askari polisi akinywa bia akiwa na sare za kazi.

Picha anazodaiwa kusambaza ni za askari polisi PC Neto Mahenge wa kituo cha polisi Mwamapalala.

"Anahojiwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na madai ya kujihusisha na vitendo vya rushwa. Nimeagiza achukuliwe maelezo na kuachiwa kwa dhamana akikamilisha taratibu na mahitaji ya kisheria," alisema Kamanda Nsimeki.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: