Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi amezindua rasmi filamu ya Ruganda iliyoandaliwa na Kikundi cha Vijana Wajasiriamali na Waigizaji Don Bosco “VIWAWADO” kwa kushirikiana na Ngama Entertainment kutoka mkoani Shinyanga.
Uzinduzi wa Filamu hiyo yenye maudhui ya kupinga mimba na ndoa za utotoni sambamba na mauaji ya vikongwe na watu wenye ualbino umefanyika usiku wa Jumapili Agosti 26,2018 katika ukumbi wa Liga Hotel Mjini Shinyanga.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Kihimbi alisema Filamu ya Ruganda imehakikiwa na ipo kwenye ubora na imepewa daraja la 16 na inaruhusiwa kuonwa na watu wa rika zote hivyo ipo kwa ajili ya jamii nzima.

“Niwapongeze sana kwa filamu nzuri kwa kweli wasanii wa Shinyanga mmeamua kuinua sanaa na kutangaza mkoa na taifa kwa ujumla ,naomba mtambue kuwa sanaa ni ajira,sanaa ni uchumi wala siyo kitu cha mzaha mzaha”,alisema.

Kwa upande wake Afisa Utamaduni mkoa wa Shinyanga,Mariam Ally alisema mandhari ya filamu ya Ruganda ni kata ya Mwamalili katika Manispaa ya Shinyanga na kwamba imelenga kuelimisha,kuonya,kuasa na kufundisha jamii kuhusu masuala ya ndoa na mimba za utotoni pamoja na kupiga vita mauaji ya vikongwe na watu wenye ualbino.

Filamu ya Ruganda ni filamu ya pili kuzinduliwa mkoani Shinyanga baada ya ile ya Nyama ya Ulimi ambazo zote zimechezwa na kutengenezwa kwa ubora wa kimataifa.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

NIMEKUWEKEA PICHA 52 ZA MATUKIO WAKATI WA UZINDUZI WA FILAMU YA RUGANDA
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi akizungumza wakati wa uzinduzi wa filamu ya Ruganda katika ukumbi Liga Hote Mjini Shinyanga Agosti 26,2018 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Wadau wa sanaa wakiwa ukumbini
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi akizungumzana wadau wa sanaa mkoani Shinyanga
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi akikata utepe ishara ya kuzindua filamu ya Ruganda 
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi akionesha  filamu ya Ruganda
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi akionesha  filamu ya Ruganda
Muonekano wa DVD 'Filamu ya Ruganda'
Waigizaji katika Filamu ya Ruganda wakicheza ukumbini
Waigizaji katika Filamu ya Ruganda wakicheza ukumbini
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi akifurahia jambo ukumbini
Afisa Utamaduni mkoa wa Shinyanga,Mariam Ally akizungumza ukumbini
Wadau wa sanaa wakiwa ukumbini wakishuhudia uzinduzi filamu ya Ruganda 
Muigizaji katika filamu ya Ruganda ' Queen' akisoma risala ya Kikundi cha Vijana Wajasiriamali na Waigizaji Don Bosco “VIWAWADO” kwa kushirikiana na Ngama Entertainment walioandaa filamu ya Ruganda
Mshereheshaji 'MC Ice' akifanya yake ukumbini
Baadhi ya Wafadhili wa filamu ya Ruganda wakiwa wamesimama
Wadau wakiwa ukumbini
Msanii Sisha akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa filamu ya Ruganda
Sisha akitoa burudani ukumbini
Sisha akiendelea kuimba ukumbini
Wachezaji wa ngoma ya zeze wakitoa burudani
Burudani kutoka WIWAWADO
Mchina Bongo (kulia) na mwenzake wakitoa burudani
Msanii 'Mzee Kiwele Wele' akisoma shairi
Picha ya pamoja,Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi na waigizaji filamu ya Ruganda
Picha ya pamoja,Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi na  wadau mbalimbali
Share To:

Anonymous

Post A Comment: