Makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula atazindua kampeni za uchaguzi mdogo wa Monduli, Jumatano Agosti 29, 2018.

Mangula atazindua kampeni za CCM Monduli mjini  katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Septemba 16.

Katibu mwenezi wa CCM Mkoa Arusha, Shaaban Mdoe amesema tayari maandalizi ya uzinduzi wa kampeni yamekamilika.

"Makamu mwenyekiti wetu (Philip) Mangula ndiye atazindua kampeni na tunaomba wanaCCM kujitokeza ili kuonyesha umoja na mshikamano wetu," amesema.

Mgombea ubunge wa CCM, Julius Kalanga amesema amejiandaa na wana CCM kutetea jimbo hilo ambalo alijiuzulu akiwa mbunge wa Chadema.

"Tutazindua kampeni Jumatano na nina uhakika wa ushindi kwani CCM ni chama imara ambacho kinakubalika sana Monduli," amesema.

Katika uchaguzi wa Monduli vyama vinane vinashiriki Chadema wamempitisha kugombea diwani wa Lepurko, Yonas Laizer.

Kata hiyo ndiyo anakotoka Kalanga ambaye pia alikuwa diwani wa kata hiyo hadi mwaka 2015 akiwa CCM na kujiunga na Chadema.

Wagombea wengine katika jimbo hilo ni Omar Kawanga (DP), Feruzi Juma (NRA), Simon Ngilisho (Demokrasia Makini), Fransis Ringo (Aada-Tadea), Elizabeth Salewa (AAFP) na Wilfred Mlay (ACT-Wazalendo)
Share To:

msumbanews

Post A Comment: