Thursday, 2 August 2018

MZIKI UNALIPA:Jay-Z na Beyoncé waingiza Tsh bilioni 198 kwa show 18 za ziara yao ya muziki ya ‘OTRII’

Wasanii wawili wenye ushawishi mkubwa duniani kwa sasa, Jay-Z na mpenzi wake Beyonce imeripotiwa kuwa wameingiza kiasi cha dola za kimarekani milioni $87 ambayo ni sawa na tsh bilioni 198 kwenye ziara yao ya OTRII inayoendelea barani Ulaya.
Image result for OTRII Beyonce Jay z
Jay-Z na Beyonce
Ziara hiyo imeingiza mkwanja huo kwa wawili hao katika show 18 walizofanya katika miji tofauti tofauti barani Ulaya ambapo bado show 30 kukamilisha ziara hiyo barani Amerika ya Kaskazini.
Kwa hesabu za kawaida Jay-Z na Beyonce kwa kila show wameingiza kiasi cha dola milioni $5.6 sawa na Bilioni 13 za kitanzania.
Ziara ya OTR II imeanza mwezi June 6 hadi Julai 17 barani Ulaya na tayari imeshaanza barani Amerika Kaskazini ambapo inatarajiwa kumalizika Oktoba 2, 2018 nchini Canada.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: