Na Frankius Cleophace Tarime.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara Samwel Kiboye No3 amewataka wananchi Wilayani Tarime Mkoani Mara kudumisha amani katika Uchaguzi mdogo wa kata ya Turwa Halmashauri ya Mji wa Tarime.

Mwenyekiti huyo amesema hayo baada ya Mkutano wa kampeni jana uliofanyika katika Viwanja vya Soko la Rebu Mjini Tarime ambao umeudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima, Mbunge wa Geita Vijijini  Joseph Kasheku (Msukuma) , na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la ukonga Mwita Waitara ambaye kwa sasa amejiunga na Chama cha Mapinduzi.

Kiboye amesema kuwa wao kama viongozi hawatakubali Wananchi kufanya fujo bila kujalai itikadi za vyama bali wananchi hao waende kupiga kura na kisha kuondoka Nyumbani kwa ajili ya kusubili Matokeo.

“Tumewakataza Vijana wa CCM Wasifanye fujo hivyo hatutafumbia Macho pia Vijana wa Vyama vya Upinzani watakaofanyafujo lazima amani itawale Tarime Uchaguzi ufanyike kwa amani” alisema Kiboye.

Samweli ameongeza kuwa wananchi wamchangue mgombea anayetokana na CCM Mwita Ghati kwa sababu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anachapa Kazi kwani Diwani huyo atafanyakazi bila kujali itikadi za vyama kama Rais wa Tanzania anavyofanya kazi kwa watanzania wote bila kujali waliomchagua na ambao hawakumchagua.

Kwa upande wake Mwita Waitara ambaye alikuwa Mbunge wa Ukongo kupitia CHADEMA amesema kuwa ameamua  kwenda CCM bila kushikinikizwa na Mtu yeyote badala ya Chama chake kushindwa kusiliza Mapendekezo yake  huku akidai kuwashughulikia Viongozi wanatokana na CHADEMA kuanzia ngazi ya taifa hadi tawi wakiwemo Wabunge wa Upinzani.

Aidha Mbunge wa Geita Mjini Joseph Kasheku (Msukuma) amesem akuwa watanzania walikuwa wanataka Mabadiliko pamoja na huduma za kijamii assa zimefanyika na zinaendelea kufanyika kwa kasi  hivyo amewataka Wanachama Wapinzania  kurudi CCM.

Uchaguzi mdogo wa Turwa unatarajia kufanyika Agost 12 Mwaka huu baada ya aliyekuwa diwani wa kataya Turwa CHADEMA Zakayo Chacha Wangwe kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: