Friday, 24 August 2018

Msanii Shilole Kapata Dili Jingine Kubwa Kutoka TTCL

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Shilole ameendelea kuneemeka kwa kupata madili makubwa kwa mwaka huu ambapo amepata dili lingine na shirika la kizawa la simu za mkononi la TTCL.

Shilole amethibitisha dili hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika; "Asanteni sana TTCL Tanzania kwa kuniamini na kunipa Nafasi hii! Mkataba umeshasainiwa. Asante Kaka yangu Waziri kwa kuniamini pia. Sasa turudi Nyumbani mashabiki zangu. #RudiNyumbaniKumenoga .Wakati ndio huu! @ttcl_corporation".

Hili ni dili la pili kwa mwaka huu kwa msanii Shilole kusaini, mwezi uliopita alisaini dili la ubalozi na British Council ambalo mwenyewe alidai kuwa ni dili nono.Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: