Wednesday, 1 August 2018

MKWASA AKIMBIZWA HOSPITALI KWA MATIBABU
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesafiri kuelekea India kwa ajili ya matibabu.
Taarifa zinaeleza kuwa, Mkwasa amesafirishwa kuelekea nchini huko kutokana na matatizo ya kiafya ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
 
Afisa habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram ameandika amemtakia kheri Mkwasa katika safari yake ya India kwa ajili ya kufanyiwa matibabu.
Mkwasa alitangaza kuachia ngazi ya Ukatibu Mkuu hivi karibuni akieleza kuwa hawezi kuwajibika kuendelea kuitumikia Yanga ili kulinda afya yake.
Mkwasa ametangazwa kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo mnamo Februari 1 mwaka 2017 na kujaza nafasi iliyoachwa wazi kwa muda mrefu iliyokuwa ikikaimiwa na Baraka Deusdedith baada ya kuondoka kwa Dkt. Jonas Tiboroha.Charles Boniface Mkwasa aliyepata nafasi ya kuichezea Yanga kwa mafanikio makubwa aliwahi pia kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kabla ya kuwa kocha wa Taifa Stars.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: