Mkurugenzi  Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Godfrey Mwambe amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwamo wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa na mawaziri kuacha kutoa matamko na maagizo kwa wawekezaji nchini.

Amesema ni vema kila mamlaka ikatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kufafania iwapo kuna tatizo lolote likiwemo la kodi,vibali au bora wa bidhaa kwa muwekezaji yoyote haja ya kufuata taratibu za kutafuta ufumbuzi kupitia mamlaka husika badala ya kutolewa maagizo ambayo hazingatii sheria.

Mwambe amesema hayo leo jijini Dar es Saalam wakati anazungumzia ziara ambayo TIC pamoja na wadau wanaohusika na sekta ya dawa na vifaa tiba nchini ambayo waliifanya Korea Kusini na China, tuzo waliyoipata ya kushika nafasi ya pili katika Maonesho ya Nanenane pamoja na kueleza majukumu yao ya kuelimisha umma na kumasisha uwekezaji.

Hivyo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kuna wimbi la viongozi kutoa maagizo na matamko na hasa yanayohusiana na masuala ya kikodi,vibali na mambo mengine.

Amesema kwamba TIC wanafanya kazi kubwa na ngumu ya kuhamasisha wawekezaji na mitaji kuja nchini na wanatumia gharama katika kufanikisha

“Kama kuna muwekezaji yoyote ana tatizo lolote wa kufahamishwa na ni kituo cha wawekezaji.Ni jambo la kushangaza Mkuu wa Wilaya anatoa makadirio ya kodi, anatoa siku mbili kodi ilipwe wakati sheria haiko hivyo.

” Unapozungumzia suala la kodi kuna utaratibu wake na sheria zake,hivyo iwapo kuna tatizo la kikodi kwa muwekezaji kiongozi wasiliana na mamlaka husika watatafuta ufumbuzi wake.

“Kama ni suala la vibali wapo wanaohusika na vibali kwa ajili ya wawekezaji,hivyo fuata utaratibu badala ya kutoa maagizo wakati huna mamlaka ya kufanya hivyo,” amesema.

Ameongeza kwamba viongozi wote jukumu lao ni kutoa taarifa kwa mamlaka husika na si kutoa maagizo na miongozo bila kufuata taratibu.

Amefafanua kuwa TRA wapo vizuri katika kufanya shughuli zao na wanacho kitengo cha uchunguzi hivyo kama mkuu wa wilaya au waziri unahisi kodi inayolipwa na muwekezaji ni ndogo au hajalipa muda mrefu lazima utaratibu ufuatwe.

Ametoa mwito kwa viongozi wote kushirikiana na TIC katika kuhakikisha wanaendelea kuweka uaminifu kwa wawekezaji ili kifikia uchumi wakati.

Pia ameomba ngazi zote za kimamlaka kila mmoja kusimama katika mipaka yake kwani kila mmoja yupo kisheria na sababu za kueleza hayo ni kukumbusha wajibu wa kila taasisi kutekeleza majukumu yake bila kuingia mipaka ya mwingine.

Mwambe ameeleza pia atamuandikia barua Kamisha wa TRA kumueleza umuhimu wa maofisa wake wa kodi kukusanya kodi kwa wawekezaji badala ya kumuacha muwekezaji anakaa miaka saba bila kulipa kodi.

“Kuna taarifa ya hivi karibuni muwekezaji amekaa miaka saba hakudaiwa kodi,anakuja mwingine mpya ndio anadaiwa na ile kodi ya miaka ya nyuma.Huu ni uzembe.

“Kwanini miaka yote ofisa wa TRA hawezi kwenda kukusanya kodi?Huo ni uzembe, nitahakikisha nasimamia hili kwa kuzungumza na Kamishna wa kodi,” amefafanua.Mwambe na kusisitiza lazima TRA wakusanye kodi.

Kuhusu ziara ya Korea Kusini na China,amesema Agosti 10 had I 18 mwaka hui aliongoza ujumbe wa wadau wanaohusika na dawa na vifaa tiba wakiwamo Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA)pamoja na Chama cha wenye viwanda vya dawa za binadamu na vifaa tiba.
 
Mwambe amesema Agosti 13 wakiwa Korea Kusini walifanya kongamano ambalo lilihusisha zaidi ya kampuni 100 wanaohusika kwenye eneo na pia wanafanya kongamano China.

Amesema matokeo ya ziara hiyo kuna kampuni tano ambazo zinahusika na uzalishaji dawa na vifaa tiba watakuja nchini Septemba mwaka huu kwa ajili ya mazungumzo kwani wanataka kuwekeza hapa nchini.

“Kampuni zote ambazo zilishiriki wanatambuliwa na HWO na kwamba ushawishi mkubwa ulikuwa kuwahamasisha waje kufanya uzalishaji dawa na vifaa tiba nchini,” amesema.

Amesema kikubwa ambacho TIC inatamani kuona ni uwekezaji wenye tija ambazo utatoa fursa Watanzania kunufaika na kuchangamkia fursa zilizopo.

Akizungumzia ushiriki wa maonesho ya Nane nane na kwamba wanazokanda saba katika kuboresha utoaji huduma kwa wadau na lengo lao Kubwa ni kutoa elimu kwa watanzania.

Amesema wamefanikiwa kushika nafasi ya pili katika ubora wa utoaji huduma na hasa katika kuwafikia wananchi na katika maonesho hayo waliwatembelea wajasiriamali waliokuwa kwenye mabanda mbalimbali kutoa elimu.

Kuhusu utendaji kazi wa pamoja ambapo TIC kuna kitengo maalum ambacho kinahusisha taasisi mbalimbali kwa lengo la kurahisisha utoaji huduma kwa wawekezaji kwa haraka.

Amesema kutokana na uwepo wa kitengo hicho wamekubaliana na NIDA nao wawepo ndani ya kituo hicho na tayari maofisa wawili wa NIDA wamewasili hapo.

Hivyo amesema wawekezaji wote wanaohitaji vibali vya NIDA watavipata TIC.Pia ameelezea umuhimu wa kuwawezesha wajasiriamali waliopo nchini kwani ndio muhimili wa maendeleo ya nchi.

Amesema nchi nyingi ambazo zimefanikiwa ni kwasababu ya wajasiriamali na kwamba TIC wanataka kuona wajasiriamali wanashiriki katika shughuli mbalimbali baada ya wawekezaji kuingia.

Amefafanua kwa mtazamo wake haoni sababu ya Dangote kuingiza magari 600 kwa ajili ya kubeba saruji, kwani hilo lilipaswa kufanywa na watanzania.

Ameongeza haiwezekani Dangote ahangaike kuzalisha saruji na wakati huo huo anahangaika na kusafirisha saruji.

Amesema jukumu muwekezaji baada ya kuzalisha kazi inayofuata ni watanzania kuchangia fursa hizo.

“Watanzania waamke na waone kuna fursa nyingi ambazo wakizitumia vizuri zitasaidia kuendeleza shughuli za kiuchumi,” amesema.

Pia amesema jukumu lao TIC ni kuendelea kutoa elimu kwa wajasiriamali ikiwa pamoja na kuwajengea uwezo na kuwaunganisha na na lengo ni kuwaunganisha na kampuni kubwa.

“Malengo ya Rais ni kuona Watanzania wanafanikiwa na ndicho ambacho hata TIC nasi tunakisimamia,” amesema.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: