Thursday, 16 August 2018

MHE. SANZIYOTE ATETEKELEZA AHADI YA KUJENGEA UWEZO VIKUNDI 40 VYA UJASIRIMALI KATIKA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA.Diwani Viti Maalum katika halmashauri ya Jiji la Mwanza Mhe. Sikitu Sanziyote ametekeleza ahadi aliyoitoa wakati wa uchaguzi ya kuweka mpango madhubiti wa kuvijengea uwezo vikundi vya ujasirimali na sanaa katika halmashauri ya Jiji la Mwanza uliogharimu shilingi 2,000,000.00 za kitanzania pamoja na mafunzo.

Mhe Sanziyote amebainisha hayo alipokuwa akikabidhi cheti cha usajiri kwa kikundii cha vijana wasanii wa  uigizaji cha Umoja Arts Group kutokea kata ya Isamilo hivi leo ambacho kinatimiza idadi ya vikundi 40. Amesema  vikundi vyote 40 vilivyonufaika na zoezi hilo vimetoka kata zote za halmashauri ya Jiji la Mwanza na vingine vipya vipo katika mchakato wa usajiri.

Mhe Sanziyote amefafanua vikundi vyote vilivyonufaika na mchakato huo vimepata mafunzo ya uandikaji wa katiba, fedha taslimu 30,000 ya usajiri, 20,000 ya ufunguaji wa kitabu cha Bank kwa kila kikundi ambayo imegharimu shilingi 2,000,000. Fedha hizo ni nje mafunzo ya ujasirimali ambayo vimepewa ikiwa ni kuviwezesha kuingia katika mchakato wa kupata tengo la 10% fedha halmashauri ya Jiji ikiwa 5% Wanawake 5% Vijana.

Naye Diwani kata ya Isamiro Mhe Charlse Nyamasiriri amempongeza Mhe Sanziyote kwa kutekeleza kwa vitendo harakati zake za ujenzi wa uchumi wa Wanawake,  kwa Vijana wa Nyamagana hususani wa Kata ya Isamiro.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿

No comments:

Post a Comment