Saturday, 4 August 2018

MBUNGE MBARAKA DAU ASEMA MAFIA SASA MAMBO NI MOTO


Sera Ya Nchi  Inataka Kila Kijiji Kuwa Na Kituo Cha Afya, Lakini Hali Hiyo Ni Tofauti  Wilaya Ya Mafia Ambapo Imekuwa  Ikikabiliwa Na Changamoto Za huduma  Ya  Afya  Kwa Kukosa Kituo Cha Afya Ata Kimoja Katika katika kata 8 Vilivyopo Wilayani hapa.                                                                                           
Mbunge wa Mafia Mbaraka Dau Ameipongeza Serikali Ya Awamu Ya Tano Kwa Kuiwezesha Wilaya Ya Mafia Kupata Kiasi Cha shilingi bilioni 22 Ambazo Zitatumika Katika Miradi Mbalimbali Ya Maendeleo Wilayani Humo.

Akizungumza Na Wakazi Wa Kijiji Cha Bweni Katika Mkutano Wa Hadhara Dau Amesema Serikali Ya Awamu Ya tano Imetoa Kiasi cha Shilingi Milioni  500 Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Kituo Cha Afya Katika Kata Ya kilonge.

Kituo Icho Cha Afya Kitakachokuwa Na Uwezo Wa Kutoa Huduma Za Mama Na Mtoto, Upasuaji Na Chumba Maaluma Cha Kujifungulia Kwa  Ajili Yakina Mama Wajawazito.

‘’ Hospitari Yetu Ya Wilaya Imekuwa Katika Changamoto Nyingi  Sana Lakini Pia Serikali Ya Rais Magufuli Imetupatia Kiasi Cha shilingi Milioni 400 Kwa Ajili Ya Ukarabati Wa Ambao Unaendea Hivi Sasa’’ Alisema dau

Milioni Hizo 400 Zitatumika Kujenga Wodi Mbili Kwa Ajili Ya Wagonjwa Wanaotumia Bima Ya Afya, Ambapo Awali Kulikuwa Na Changamoto Ya Kukosekana Wodi Maalum Ya Wagonjwa Wanaotumia bima Ya Afya Na Wasio kuwa Na bima Kupata Huduma Pamoja Hali Iliyokuwa Inasababisha Usumbufu Kwa Wananchi.

Aidha Mbunge Uyo ametoa Vifaa Mbalimbali Katika Zahanati Ya Bweni Iliyokuwa Ikikabiliwa Na Ukosefu Wa Vifaa Tiba Vya Maabara Pamoja Na Madawa Na Mashuka Kwa Ajili Ya Wagonjwa Wanaolazwa Katika Zahanati Hiyo Ya Bweni.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: