Saturday, 4 August 2018

MBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA KUINUA TASNIA YA MICHEZO


Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula ameiambia radio Lake Fm baada ya miradi yote ya Maendeleo iliyopo kwenye Ilani ya uchaguzi  2015-2020 kuwa katika hatua za utekelezaji, na michache kukamilika na baadhi yake kuwa katika mpango, sasa yupo tayari kurejesha mashindano mbali mbali ya mpira wa Miguu,  Pete na kikapu, Draft pamoja na Nyavu yatakayo kuwa na hadhi ya kijimbo, na tayari katika ramadhani hii alianza na Mabula Ramadan Championship Cup 2018.

Mhe Mabula ametoa ufafanuzi huo akijibu swali katika mahojiano maalum alipopata fursa ya kutembelea Radio ya kanda ya ziwa Lake Fm, lililohoji nini hatma ya ukimya wa Mashindano yaliyokuwa yamebeba jina lake alipokuwa Mayor.

Imetolewa na
Ofisi Ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: