Mh. Stanislaus Mabula Mbunge Jimbo la Nyamagana kuanzisha tuzo maalumu ya wanawake mahususi kutunuku  wajasirimali na wawekezaji wanawake, ili  kuenzi jitihada na harakati za kufikia uchumi wa viwanda kwa mstakabali wa ujenzi wa Maendeleo Nyamagana na taifa kwa ujumla

Haya yamebainishwa na katibu wa taasis ya First community organization Bi Florah Magabe akimwakilisha Mgeni Rasmi, Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula  katika kongamano maalumu la uchumi, uwekezaji na mahusiano lililoitwa Red and Silver Party JB Belmond Hotel. Bi Magabe alitumia adhara hiyo kutoa salamu za Mhe Stanislaus Mabula kwa kupongeza kikundi cha 'Mwanamke Mpambanaji' Kwa harakati zake za ujenzi wa fikra mpya za kiuchumi, kupitia kongamano lenye dhima ya kuwatoka wanawake na Vijana na wana Mwanza katika fikra za uchuuzi na kwenda katika ujasirimali na uwekezaji ili kufikishwa adhima ya uchumi wa viwanda.

Bi Magabe alifafanua, Mbunge Jimbo la Nyamagana anatambua jitahada kubwa za wanawake katika kufikia  uchumi viwanda  Nyamagana kupitia harakati za elimu ya ujasirimali ili kutoka dhana ya kichuuzi, kufikia  ujasirimali na uwekezaji. Mhe Mabula katika kwenda sambamba na dhima ya serikali ya CCM inayoogozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli  ya uchumi wa viwanda,  amedhamiria kuanzisha Tuzo maalumu ya kutunuku  wanawake kila mwaka, Kutoa mafunzo ya ujasirimali, uandikaji miradi na mpango wa Biashara na masoko  kwa ushirikiano na taasis ya First community ili kutambua na kuenzi mchango, jitihada na harakati za wanawake katika kukuza pato lao, halmshauri na taifa ili kufikia uchumi wa Kati ambao ni wa viwanda. 

Naye katibu wa Mbunge Jimbo la Nyamagana Ndg Heri Nkoromo Kipara amesema ofisi ya Mbunge imewezesha kusaidia usajiri wa vikundi katika halmashauri ya Jiji la Mwanza vipatavyo 375. Amepongeza kikundi cha Mwanamke Mpambanaji kujisajairi. Kadharika Ndg Heri amefafanua kuwa katika tengo la fedha 10% ya halmshauri Jiji la Mwanza 80% wanawake wameonesha nidhamu ya jedwari la marejesho na fedha hiyo kufanya Kazi iliyokusudiwa.  Hivyo wanawake ninguzo kubwa katika ujenzi wa pato la taifa. Hivyo ofisi ya Mbunge itakuwa tayari kushirikiana na vikundi vyote vilivyosajiriwa halmashauri ili viweze kunufaika na tengo la 10% ambalo ni halali kwa Vijana na wanawake.

Naye Ndg Irene Mbowe mwezeshaji wa kitaifa na kimataifa alitumia jukwaa hilo kuhasa jamii ya kitanzania kufuata maadili na utamaduni za kiafrika kwa wanawake kutokebehi Maumbile ya wanaume kwakudhiki kupitia taswira matunda au mboga. Amewaasa wanawake kusimama katika nafasi ya utu wema, upendo, nidhamu na heshima kwa familia zao sanjali na kujihusisha na shughuli za ujasirimali na uwekezaji ili kujitegemea na kuondokana na dhana ya utegemezi.

Naye Mwenyekiti wa kikundi cha 'Mwanamke Mpambanaji' Bi Paulina Francis alimshukuru Mhe Mabula kwa utayari wa kuwa mgeni rasmi sanjari kuwa mstari wa mbele kuunga jitihada za ukombozi wa wanawake kiuchumi ili kuwa nguzo katika ujenzi wa pato la wanawake na taifa. Kogamano hilo lilipambwa na wasanii wa kizazi kipya,  wakufunzi wa Biashara na uchumi,  pychologist, mahusiano pamoja na chakula cha Usiku.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana 🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: