Friday, 17 August 2018

MBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA APOKEA MIFUKO 230 YA SARUJIMdau wa maendeleo Mwanza Huduma aunga jitahada zinazofanywa na Mbunge Jimbo la Nyamagana katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa kutoa mifuko  230 ya Saruji.

Akikabidhi mifuko hiyo ya Saruji Ngd. Zolfikar Nanji amesema amefarijika kuona harakati za maendeleo zinazofanywa na Mbunge Jimbo la Nyamagana pamoja na serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu,  hivyo amekabidhi mifuko ya Saruji 230 yenye thamani ya shilingi 4,025,000.00  ambapo kila mfuko ni shilingi 17500.

Naye Mhe. Stanslaus Mabula amepongeza Mwanza kuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali ya CCM chini ya Jemedari Mhe Dkt John Pombe Magufuli ambayo imekusudia kufikisha huduma karibu na wananchi. Na Kwa kukabiliana na changamoto sekta ya Afya mifuko yote itapelekwa Kanindo, Mbugani, Nyegezi Nyabulogoya, Kata ya  Butimba katika hospitali ya wilaya pamoja na Kata ya Mhandu.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿

No comments:

Post a Comment