Saturday, 25 August 2018

Mbunge Jimbo la Nyamagana afungua michuano ya ligi daraja ya nne ungwe ya pili 2018


Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanislaus Mabula  amefungua rasmi michuano ya ligi daraja la nne ungwe ya pili wilaya. Ikiwa ni mashindano yaliyoandaliwa na Chama Cha Mpira wa Mguu wilaya "NDFA" (Nyamagana District Football Association) 2018.

Akimwakilisha Mhe. Mabula Mwenyekiti wa taasis ya First Community Organisation Ndg. Ahmed Misanga amewapa salamu za Mhe Mbunge na utayari wake katika kufadhiri michuano  kwa vifaa vyote vya michezo pamoja na zawadi ili kuleta hamasa na hadhi ya mashindano haya kiwilaya. Hivyo ametumia adhira hiyo kuwatakia mashindano mema katika ushindani unaozingatia maadili na sheria 17 za michezo.

Ungwe hii ya pili inakutanisha Vikosi Tisa ikiwa ni Talent Red, AFC Lumumba, Machinga FC, Small Boys, Wajasiri, Nyamagana FC, Kangaye FC, Mwanza City FC pamoja na Black Lion FC ambavyo vimefuvu ungwe ya kwanza iliyovihusisha vikosi 27. Katika michuano hii washindi wa kwanza na wapili watashiriki michuano ya kimkoa, pamoja na kuzawadiwa kikombe na fedha taslimu shilingi 500,000 kwa mshindi wa kwanza, shilingi 200,000 na kikombe kwa mshindi wa pili, mipira miwili kwa mshindi wa tatu, kiatu cha dhahabu kwa mchezaji bora na 50,000 na shilingi 50,000, jezi na box la uwamuzi kwa mwamuzi bora

Katika mechi ya ufunguzi ungwe ya pili kikosi cha Talent FC kiligarazwa gori tatu bila  na kikosi cha Lumumba FC. Mechi ya pili Wamachinga FC  ilitamba dakika 90 kwa gori tatu bila kwa kikosi cha Small boy FC.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: