TUME YA NGUVU ZA ATOMU TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA


Arusha 14 Agosti, 2018

Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania kwa ushirikiano na Jumuia ya Umoja wa Ulaya (EU) imefanya mafunzo ya siku mbili ya namna ya kutafuta na kuvibaini vyanzo vya mionzi vilivyopotea au kutelekezwa. Mafunzo haya yaliyohitimishwa leo, yalianza jana tarehe 13 Agosti, 2018 Makao Makuu ya Tume Jijini Arusha.

 Mafunzo haya yalifanyika kwa vitendo juu ya namna ya kuweza kubaini na kutambua vyanzo vya mionzi vilivyotelekezwa au kupotea ili kuhakikisha vinahifadhiwa katika mazingira ya kiusalama. Jumla ya washiriki 15 kutoka nchi jirani za Zambia, Malawi waliudhuria mafunzo haya wakiongozwa na mwenyeji Tanzania 
Lengo kuu la zoezi hili lilikuwa ni kutoa ufahamu na uelewa juu ya kubaini vyanzo vya mionzi vilivyopotea, kufanya maandalizi ya dharura pindi matukio ya  kinyuklia yanapotokea pamoja na jinsi ya kutumia vifaa vya kubainia  mionzi.

Maarifa yaliyopatikana kupitia mafunzo haya  yataimarisha uwezo wa kiufundi katika nyanja tofauti za usalama wa nyuklia, hasa utambuzi, na hatimaye uhifadhi salama wa vyanzo vya mionzi  ili kulinda umma na mazingira dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na vyanzo vya mionzi.

Imetolewa na;
Peter G. Ngamilo, Kitengo cha Masoko na Mawasiliano
Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania
Share To:

msumbanews

Post A Comment: