Monday, 6 August 2018

KISA BOKO-Wakinamama Mafia Wajifungulia Manyumbani


Wakazi wa Kijiji Cha Chunguluma Wilaya Ya Mafia Wamepaza Sauti Zao Kwa Kuiomba Serikali Kuwadhibiti Wanyama Aina Ya Viboko Wanaofanya uharibifu  Wa Mazao Pamoja Na Mali Na Kutishia Usalama Wa maisha Yao 
Wakizungumza Wakati Wa Mkutano Wa Hadhara Ulioitishwa Na Mbunge Wa Jimbo Ilo Mhe. Mbaraka Dau Wananchi Hao Wamemuomba Mbunge Wao Kuhakikisha Anamaliza Changamoto Hiyo Kwa Kuwa Imefikia Wamama Wajawazito  Wakijifungulia Manyumbani Kwa Kuhofia Kushambaliwa Na Viboko.

‘’Mheshimiwa Mbunge Hapa Tunatatizo Kubwa Sana La Wanyama Viboko Wanatufanya Tunalala Saa 12 Jioni Na Tunashindwa Kutembelea Usiku Kwa Hofu Ya Boko Wanatembea Hovyo Juzi Usiku Mama Mwenzetu Kajifungulia Nyumbani Kwa Sababu Ilikuwa ni Usiku Kwa Hofu Ya Kukutana na Viboko Akalazimika Kujifungulia Nyumbani ’’ Alisema Arafa Mchungu
Pamoja Na Tishio La Usalama Wao Boko Hao wamekuwa Wakifanya Uharibifu Wa Mazao Mashambani hali Inayowatia Umasikini Mkubwa

Nae Bwana Mohamed Kombo amedai Viboko Hao Wamebadilisha Mfumo Wa Maisha Yao Kwa Kupandisha Gharama Za maisha Kwa Kuwa Vijana Wa Bodaboda Wamekuwa  Wamepandisha Nauli Asa Nyakati Za Jioni Kutokana Na Tishio la Wanyama Hao.

‘’ Hivi sasa Boko Wanaendesha Uchumi Wetu Asa Kwenye Usafiri Bodaboda Mpaka Umpe Elfu 20 Ndio akupeleke Mjini’’ 
Akijibu Hoja Hizo Mbunge Wa Mafia Mbaraka Dau Amesema Ameshafanya Juhudi Mbalimbali Serikali Ipo Katika Mchakato Wa Kuwadhibiti Boko Hao Ili Wasiendelee Kuwaletea Madhara.

‘’Ndugu Wananchi Kwanza  nawapa Pole Sana Lakini,  Jambo Ili La  viboko Nilishaliombea Muongozo Bungeni Na,  Waziri Wa Maliasili Na Utalii Alileta Wataalam Hapa Chunguluma  Kwa Lengo la Kwadhibiti Wasiendelee kuleta Madhara’’ Alisema Mhe. Dau
Kisiwa Cha Mafia ni Kisiwa Pekee Dunia Ambacho Kipo Ndani ya Bahari Ya Hindi Ambapo kunapatika Wanyama Aina Ya Viboko.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: