Thursday, 23 August 2018

Kikosi cha Yanga kinachoweza kuanza dhidi ya Mtibwa leo 23.8.2018

Yanga leo inashuka Dimbani kucheza na Mtibwa Sugar mechi ya Kwanza ligi kuu Tanzania Bara TPL msimu wa 2018/2019.
Hiki ni Kikosi cha Yanga kinachoweza Kuanza dhidi ya Mtibwa Sugar.
Golini, Klaus Kindoki Mkongomani katika mechi za majaribio anaonekana ananafasi kubwa ya Kuanza leo lakini kiwango cha Beno Kakolanya alichokionyesha dhidi ya USM Alger kinaweza kumfanya Kindoki kusubiri benchi na Beno Kuanza.
Mabeki wa Pembeni , Namba 2 na 3 – Kuhusu namba mbili ni wazi Juma Abdul Mnyamani ataendelea kuaminika kwenye kikosi cha Mwinyi Zahera na namba tatu Gadiel Michael
Mabeki wa kati, 4 na 5. Hapa kuna Ukuta ambao tayari umeanza kuonekana kuzidi kuelewana Andrew Vincent na Kelvin Yondani ambao wamekuwa wakicheza pamoja muda mwingi.
Viungo wa kati, Namba 6 na 8 Namba 6 Abdallah Shaibu Ninja ambaye amekuwa na msaada mkubwa kwa mabeki wa kati Yondani na Andrew Vincent licha ya kuwa amekuwa anakosa unyumbufu kama viungo wengi lakini ni bora zaidi kwenye Ulinzi huyu anaweza kuanza leo huku namba 8 Papy Tshishimbi akiwa na nafasi kubwa ya Kuanza.
Viungo wa Pembeni : Mrisho Ngassa msomaji wa Kwataunit.co.ke anaweza kuwa na nafasi nzuri ya Kuanza kama namba 7 na 11 Deus Kaseke au Ngassa akaanzia sub then Feisal Salum akaanza kama mtu wa pembeni ambaye anacheza pia eneo la katikati ya uwanja.
Washambuliaji : Namba 9 Mtu ya Congo Heritier Makambo  ambaye anaweza kusimama na Mmoja kati ya Raphael Daud au Matheo Anthony ambaye ni bora pia kwenye nafasi ya Ushambuliaji.

No comments:

Post a Comment