Tuesday, 7 August 2018

Kigwangala amlilia Hamza Temba......Asherehekea Miaka 43 Akiwa Hospitalini

Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangala leo anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anakotibiwa.

Dk Kigwangala, leo Agosti 7, anatimiza miaka 43 ya kuzaliwa kwake. Waziri huyo alipata ajali ya gari Agosti 4 mwaka huu eneo la Magugu, Manyara.

Ameandika katika ukurasa wake wa twitter akimshukuru Mungu kwa kufikisha umri huyo.

“Leo ninatimiza miaka 43 toka nizaliwe. Ahimidiwe Allah aliye Mkuu kuwa bado nipo hai mpaka sasa. Najua ni kwa utashi na kusudio lake. Namshukuru na nazidi kuomba kwake shufaa, siha na mafanikio tele. Ninawashukuruni nyote kwa dua zenu. Tudumu kwenye sala ndugu zangu.”Ameandika.

Pia, ameutumia mtandao huo, kumkumbuka Ofisa Habari wa Wizara yake, Hamza Temba aliyefariki  dunia katika ajali hiyo.
 
“Sijui hata Kwa nini usiku huu nimegusa simu? 😭😭😭 Only to look at my phone and come across chats and pics za ziara yetu ya #PoriKwaPori and rise to the reality that mdogo wangu, bwashee wangu, this hard working, smart, handsome and very hopeful young man sintomuona tena na kumtania. What more can I say?! Alhamdulillah. Qaalu inna lillah wainna ilayhir rajiuun. 🙏🏿 #AllahAkbar“ 

No comments:

Post a comment