Friday, 24 August 2018

Kauli ya kocha wa Yanga baada ya kupata ushindi

Yanga wameanza ligi kwa kutoa kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar. Pamoja na kwamba walionekana hawako vizuri, Yanga wameonyesha soka safi na kufanikiwa kushinda kwa mabao hayo, shujaa wakiwa Kelvin Yondani na Herietie Makambo raia wa DR Congo.

Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 31, Makambo akiunganisha vizuri kabisa. Wakati ikionekana kama Mtibwa Sugar wangeweza kusawazisha, shambulizi la kushitukiza, dakika ya 39, Mrisho Ngassa aliangushwa ndani ya eneo la hatari na mwamuzi akaamuru mkwaju wa penalti upikwe.

Dakika ya 40, Yondani akaumwamisha mpira wavuni kwa ufundi maridadi akimuacha kipa Tinocco akianguka “halijojo”.

Bao pekee la Mtibwa Sugar lilifungwa na Haruna Chanongo na Yanga wakashambulia zaidi mwishoni huku Tinocco akifanya kazi ya ziada kuokoa mkwaju matata wa Ibrahim Ajibu.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: