Mapema leo katibu wa uvccm wilaya ya Shinyanga Mjini ametembelewa na Viongozi wa waendesha Daladala katika wilaya ya Shinyanga Mjini.

Pamoja na mambo mengine katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini amepokea kero na changamoto mbalimbali ikiwemo kamata kamata ya hovyo kwa waendesha Baisikeli kitu ambacho imekuwa ni kero kubwa kwa vijana hawo katibu amewahaidi kuwakutanisha na Mkuu wa wilaya pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama kuja kuwasikiliza vijana hawo kwani wanaamini hawana sehemu pa kukimbilia zaidi ya kwenye Chama chao ambacho ni Chama Tawala.

Pia katika muendelezo mazungumzo yao katibu aliwaeleza kuwa vijana mnapaswa kuwa karibu na chama Cha mapinduzi muda wote kwani msaada wenu uko ndani ya chama na sio nje ya chama mjitaidi kuunda katiba na msajili umoja wenu ili mwenzenu anapopata Tatizo hiwe ni rahisi kumsaidia.

Lakini pia katibu aliwaambia kuwa vijana sie waendesha bodaboda ndio chanzo cha kugawa Rushwa kwa Asikari ukikamatwa tu kidogo badala ya kusimamia haki yako unakubali kutoa Rushwa ili wakuachie naomba niwaonye tabia hiyo iishe mara moja, na mtu akikamatwa naomba tuwasiliane ili tuone ni njia gani ya kuwasaidia. Kuliko kuwazoesha hawa asikari Rushwa.

Mwisho.
Katibu aliwatakia mafanikio mema vijana hawo na kuhaidi kuendelea kuwapa ushirikiano .

*IMATOLEWA NA*
*OFISI YA UVCCM*
*WILAYA YA SHINYNGA MJINI*
Share To:

msumbanews

Post A Comment: