Jeshi la Polisi Kanda Maluum ya Dar es Salaam linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuteka watu na kudai fedha, watuhumiwa hao ni Hussein Shilingi  (30) mkazi wa Kimara Mwisho na Martin Pumba (35) makazi wa Tabata.

Kanda wa Kamda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema kwamba mnamo Julai 26 mwaka huu maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) watuhumiwa hao walitiwa mbaroni na walikuwa wakitumia gari yenye namba za umoja wa mataifa (UN) ambazo ni T 452 CD 639 Toyota Land Cruiser huku ndani ya gari hilo wakiwa na watu 5 waliowateka. Amesema mara upelezi utakapokamilikwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.

Katika hatua nyingine kamanda huyo ameeleza kwamba jeshi lake halitishwi na watu wanaotumia matunguli kama njia ya kujikinga kwani watashuulikiwa vilivyo na matunguli yao.

Vilevile Mambosasa amezungumzia juu ya Jeshi lake lilivyojipanga kuimarisha ulinzi na usalama katika mashindano ya michezo ya majeshi ya Polisi ya nchi za ukanda wa afrika mashariki na kati (EAPCCO GAMES 2018) yatakayofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa katika uwanja wa uhuru Agosti 6, mwaka huu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: