Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiangalia mwani katika eneo la Taasisi ya  Utafiti wa Mifugo Zanzibar, Dole Wilaya ya Maghribi "A" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo wakati alipotembelea akiwa katika ziara maalum
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya angalia mwani katika eneo la Taasisi ya  Utafiti wa Mifugo  Dkt.Kassim Gharib (wa pili kulia)  wakati alipotembelea katika eneo la Taasisi hiyo iliyopo   Dole Wilaya ya Maghribi "A" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo wakati alipotembelea akiwa katika ziara maalum
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akimuuliza suala Mtafiti wa Magonjwa na Uzalishaji Mifugo Dkt.Waridi Abdulla Mussa (kulis) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti huyo alifikas kuasngaslias kuku wa asili (kienyeji) akiwa katika ziara ya kutembelea  katika eneo la Taasisi ya  Utafiti wa Mifugo  Dole Wilaya ya Maghribi "A" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiuliza suala kwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Ardhi Ahmed Abrahmani Rashid (kulia) alipofika kutembelea Eneo la ujenzi wa Hospitali kubwa ya Rufaa inayotarajiwa kujengwa Binguni  Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja  leo akiwa katika ziara maalum,(katikati) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Hassan Khatibu Hassan
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Hassan Khatibu Hassan(kushoto) alipotembelea Eneo la ujenzi wa Hospitali kubwa ya Rufaa  inayotarajiwa kujengwa Binguni Katika  Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo (kulia) Mhe.Haji Omar Kheir Kaimu Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idare malum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheri. 
Picha na IKULU


Na Faki Mjaka, Maelezo Zanzibar 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amesema azma ya serikali anayoiongoza ni kuhakikisha kuwa tafiti za Mifugo na Afya zinafanyika Zanzibar badala ya kufanyika nje ya Zanzibar.
Amesema kuundwa kwa Taasisi za kitafiti na kujengewa uwezo Taasisi hizo ni hatua muhimu itakayo chochea kasi ya maendeleo na kupunguza gharama.
Rais Shein ameyasema hayo alipofanya ziara katika eneo la Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Dole Wilaya ya Magharibi A na eneo la Binguni ambapo Hospital ya Rufaa itakayojumuisha Taasisi ya Utafiti ya Afya inajengwa.
Akiwa katika Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Dkt Shein ameridhishwa na maendeleo ya Taasisi hiyo ikiwemo ukarabati wa majengo mbalimbali na shughuli za kitafiti zinazoendelea katika Taasisi hiyo.
Dkt Shein alijionea Tafiti zinazoendelea katika Taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na ufugaji wa kuku wa Kienyeji na chakula cha Samaki.
Aidha ameahidi kuendeleza mashirikiano yake kwa Taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kusaidia kuiwezesha kifedha ili kukidhi bajeti ya Taasisi hiyo.
Akiwa Binguni Dkt. Shein aliweza kukagua mipaka ya eneo ambalo Hospital ya kisasa ya Rufaa inatarajiwa kujengwa.
Amezitaka Taasisi zinazohusika na eneo hilo kuhakikisha wanafanya marekebisho ya upimaji wa eneo hilo ili kurahisisha ujenzi wa Hosptiali hiyo.
Ujenzi huo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambapo Dkt Shein aliahidi kuijenga Hosptal hiyo katika mikutano ya kujinadi kuchaguliwa.
Akielezea kwa undani Dktk Shein amesema Tayari Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshaomba Fedha za Mkopo na kwamba kila kitu kimeenda sawa hivyo ujenzi unaweza kuanza mara tu fedha zitakapopatikana.
Dkt Shein amewataka Wananchi kujitolea kwa hali na mali ili kufanikisha ujenzi huo pale utakapo anza.
Katika Ujenzi huo kutakuwa na Hospital ya Rufaa na Taasisi ya Utafiti wa Afya na nyumba za Wafanyakazi.
Awali akitoa Salamu za Kichama Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Dkt Abdallah Sadala amempongeza Dkt Shein kwa kuendelea kuitekeleza vyema Ilani ya CCM kama alivyoahidi kwa wananchi na hivyo kuomba wananchi waendelee kumuunga Mkono.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: