Tuesday, 21 August 2018

Diwani wa CCM kata ya Nyankumbu afariki dunia


Diwani wa kata ya Nyankumbu, (CCM) Wilayani Geita, Michael Kapaya amefariki dunia leo Agosti 21,2018.

Kapaya amefariki dunia wakati akipata matibabu hospitali ya Mkoa ya Geita.

Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya mji wa Geita Leornad Bugomola amesema diwani huyo amefariki leo saa 4 asubuhi.

Akizungumza kwa njia ya simu Bugomola amesema taarifa za msiba amezipata akiwa Chato kwenye mazishi ya dada yake Rais John Magufuli.

“Baada ya kumaliza shughuli za mazishi tutarudi Geita mjini kupanga taratibu za msiba wa Diwani huyo,” amesema

Na Rehema Matowo, Mwananchi

No comments:

Post a Comment