Diwani wa kata ya Kia kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Ndg. Yohana Laizer ametangaza kujiuzulu nyadhifa zake zote na kujiunga na Chama cha Mapinduzi Ccm mapema hii leo.

Ndg Laizer amechukua maamuzi hayo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kia Mh.Lengai Ole Sabaya kufanya ziara katika kata ya kia kwa ajili ya kutatua kero mbalimbali za wananchi katika kata hiyo baada ya kutatua kero hizo Diwani huyo aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kufurahishwa na kazi nzuri anazofanya Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na serikali ya awamu ya tano.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: