Na James Timber, Mwanza
Waendesha pikipiki maarufu Bodaboda jijini Mwanza wamekuwa msaada katika suala la Ulinzi na Usalama kutokana na kuwepo kwa taarifa nyingi kutoka kwa madereva hao  juu ya watu wanaohisiwa  wakishiriki vitendo vya kuhatarisha amani.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk. Philis Nyimbi katika Semina ya iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma wa Nishati na Maji (EWURA CCC), amesema kuwa madereva hao waongeze juhudi kwa kutoa ushirikiano kama ilivyo sasa.

Kwa upande wake Katibu wa (EWURA CCC) nchini Mhandisi Goodluck Mmari, amesema lengo la elimu hiyo ni kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma za Maji na Nishati na mahitaji mengine yanayodhibitiwa na EWURA.

Mhandisi Mmari amesema kuwa katika elimu hiyo wamelenga kundi la boda boda kutokana kuwa wao ndio watumiaji wakubwa wa Nishati na Maji, huku akiwataka washiriki hao kulipa ankara kwa wakati ili kuboreshewa huduma hizo ikiwemo kuwafichua wanao hujumu miundombinu.

Naye Mwenyekiti Mkoa wa Mwanza (EWURA CCC), Peter Niboye  ametoa rai kwa washiriki hao kusambaza elimu waliyoipata kwa wadau mbalimbali na jamii kiujumla  juu ya haki na wajibu katika matumizi ya nishati na maji jijini hapa.

Aidha moja kati ya baadhi ya washiriki katika semina hiyo Makoye Kayanda ameipongeza EWURA kwa kufanya kazi vizuri na ufanisi kwa faida ya watumiaji.

Hata hivyo Makoye ameiomba EWURA kufuatilia baadhi ya sheria zinazowekwa katika vituo vya mafuta ambazo siyo salama kwa mteja, huku  akitolea mfano wanaoenda na abiria kuongeza mafuta huku wakielekezwa kulipia huduma hiyo kupitia miamala ya kifedha jambo ambalo lina hatarisha maisha ya abiria na wahudumu katika kituo hicho kwani tahadhari kila kituo wamedhibiti matumizi ya simu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: