Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh. Jerry Cornel  Muro ametoa mwezi mmoja kwa wanaume waliotelekeza watoto wilayani humo  kuhakikisha wanaanza kutafuta watoto wao  na kuanza kuwahudumia .

Dc Muro Alisema baada ya muda aliotoa kuisha ataanza kuwakaribisha Wanawake wote wanaoishi wilayani humo  waliotelekezewa watoto kupeleka Malalamiko yap ofisini kwake.

Muro alitoa  maagizo hayo juzi wakati Akizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya utelekezji wa watoto wilayani humor,Alisema lengo la zoezi hilo ni kupunguza idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu ,hatarishi na wanaojihusisha na uhalifu na wale wanaozurura na kuzagaa mitaani kwa kukosa malezi ya Wazazi wawili.

" Nichukue fursa hii kuwataarifu akinamama na akinadada waliozalishwa na kutelekezewa watoto na kuachwa wabebe Mzigo wa kuwahudumia watoto WAP, Natoa mwezi mmoja kwa kila mwanaume anayejua huko Arumeru aanze kutafuta mtoto aliyemtelekeza"Alisema Muro

Aidha Dc Muro Alisema licha ya serikali kutangaza Elimu bure kwa wanafunzi wako baadhi ya wanafunzi ambao wanakwenda  Shule bila sare  ya Shule madaftari au viatu huku moja ya sababu inayochangia hali hiyo ikiwa  ni kutelekezwa na baba zako.

" Nitoe rai tu najua wako watu watakaokaidi naomba wajifunze kupitia zoezi lililofanyika Dar es salaam likiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda zoezi la Arumeru nitakuwa Kali zaidi kuliko la Dar, wajue zoezi limeisha huko na limetua Arumeru Alisema.

Credit : Mtanzania
Share To:

msumbanews

Post A Comment: