Mwanamuziki wa Uganda na Mbunge wa Jimbo la Kyaddondo Mashariki, Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina la  Bobi Wine ambaye amekuwa akizuiliwa kwa karibu wiki mbili nchini humo ameachiliwa huru kwa dhamana na Mahakama Kuu mjini Gulu.
Mbunge huyo amepewa dhamana pamoja na wabunge wengine watatu, na watuhumiwa wengine wanane.
Washtakiwa hao wanadaiwa kuhusika katika kurushia mawe magari ya msafara wa Rais Yoweri Museveni wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa eneo Bunge la Arua.
Kassiano Wadri aliyeshinda ubunge Arua ni miongoni mwa wabunge waliokuwa akishikiliwa na jeshi la polisi la nchi hiyo.
Wadri ameachiliwa kwa dhamana lakini akazuiwa kuzuru eneo Bunge lake kwa miezi mitatu bila idhini ya Mahakama.
Maombi ya dhamana ya washukiwa wengine 21 walioshtakiwa pamoja na Bobi Wine yatasikilizwa na mahakama baadaye leo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: