Thursday, 23 August 2018

Mabasi ya Shule Yagongana Jijini Mwanza Na Kuua Mmoja


Basi la shule ya msingi Kivulini na la shule ya msingi Nyamuge yamegongana leo asubuhi na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Akizungumzia tukio hilo leo Agosti 23, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza(anayehamia makao makuu ya Polisi Dar,) Ahmed Msangi amesema aliyefariki ni dereva wa gari la shule ya Nyamuge Albert Joram(58).

Amesema watu wengine wanane na dereva wa gari la Kivulini Kulwa Mayala 27, wamepata majeraha sehemu mbalimbali za miili yao zaidi hasa miguuni.

“Majeruhi hao walikimbizwa katika kituo cha afya cha Buzuruga na baadae mwanafunzi mmoja alilazimika kuhamishiwa hospitali ya rufaa, Bugando kwa matibabu zaidi huku wawili wakilazwa katika hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza,”amesema.

Amesema kwa sasa hali za majeruhi zinaendelea vizuri na tayari wale wa tano wameruhusiwa ingawa wanahitaji vipimo vya kina.

No comments:

Post a Comment