Friday, 24 August 2018

Baba Afikishwa Mahakamani kwa Kubaka Mtoto wake

Mkazi wa Stendimpya, Mugumu, Nyamhura Werema (35)amepandishwa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa miaka(12)


Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile, mwendesha mashtaka wa polisi, Paskael Nkenyenge amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai mwaka huu.


“Mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 158(1) (a) cha kanuni ya adhabu sura 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002,” amesema


Amesema Upelelezi haujakamilika na mshitakiwa amekana shitaka. Mshtakiwa amenyimwa dhamana na kesi yake itatajwa tena Septemba mwaka huu.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: