Tuesday, 14 August 2018

AJALI YAUA 5 NA KUJERUHI 3 TARIME

Gari ya kubeba abiria wa Samaki kutoka Sjirati na kwenda Tarime Leo asubuhi limepata ajali na kuua watu 5 na kujeruhi wengine 3.

Kamanda mkoa wa kipolisi,Tarime na Rorya,Henry Mwaibambe amewaambia waandishi wa habari kwanjia ya simu ya kiganjani kuwa kati yao waliokufa in Dereva wa gari hill,Masiaga huku marehemu wengine majina hayaja julikana.

Mwaimbe ameingeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi baada ya dereva hiyo kusimamishwa na polisi kisha kukaidi na kisha gari kujigonga kwenye tuta(bams).

pia Mwaibambe ameongeza kuwa ajali hiyo imetokea majira ya asubuhi wakati gari likiwa linatoka Shirati kuelekea Tarime huku likuwa limebeba wafanyabiasgara wa Samaki na Samaki.


Kamanda mwaibambe amekeme tabia ya baadhi ya madereva kuendesha kwa mwendokasi.

No comments:

Post a Comment