Monday, 20 August 2018

Abiria 60 wanusurika basi latekeketea kwa moto


Abiria 60 wanusurika kifo baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Kigoma kwenda Sumbawanga mkoani Rukwa kuteketea kwa moto.
Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoani Kigoma Martin Ottieno amesema tukio hilo limetokea leo Agosti 20 eneo la Kazurambimba wilayani Kigoma.
Kamanda Ottieno amesema kwamba basi lililopata ajali hiyo  linamilikiwa na Kampuni Saratoga. 
"Hakuna abiria aliyepoteza maisha wala kupata madhara ya aina yoyote zaidi ya baadhi ya mizigo yao kuteketea kwa moto," amesema Kamanda Ottieno
Polisi wanaendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment