Saturday, 14 July 2018

Zari Ampa Pole Hamisa Baada Ya Kukanwa na Diamond Hadharani

Zarinah Hassan ‘Zari’ amerudi Kwenye headlines tena baada ya kumuandikia ujumbe adui yake namba moja Hamisa Mobetto baada ya kukanwa na Diamond hadharani.

Sakata hilo lilianza jana baada ya Diamond kuachia video yake mpya ya wimbo wake wa ‘Baila’ ambapo aliposti Kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika kuwa hajapata mwanamke wa kuwa naye lakini siku akimpata atamsikilizisha Baila:
 
"Kwa machache niliyojifunza Kwenye Mahusiano nilisema siku nikikutana na mwanamke mpya nitakayetaka kuwa naye kabla ya kuianza Safari sitamwambia neno bali nitamuwekea huu wimbo wa Baila”.

Baada ya Diamond kuweka wazi kuwa hayupo kwenye mahusiano moja kwa moja Zari alianza kumnanga Hamisa na kumpa pole baada ya kukataliwa na mwanaume ambaye amekuwa akijitangaza kuwa Kwenye Mahusiano naye.

Kwenye ukurasa wake wa Snapchat Zari aliandika maneno ambayo directly alikuwa anampiga vijembe Hamisa na kumcheka kuwa amekaa Kwenye Mahusiano na mwanaume kwa miaka kumi lakini bado anamkana hadharani kuwa hana uhusiano naye:

Bifu la Zari na Hamisa lilianza baada ya Diamond kuchepuka Kwenye Mahusiano Yake na Zari na kuzaa mtoto na Hamisa Mobetto tangia hapo Zari na Mobetto hawaivi chungu kimoja ni majungu kwenda mbele na kujibizana mitandaoni.

No comments:

Post a Comment