Sunday, 8 July 2018

Wenyeji Urusi Waaga Mashindano Ya Kombe La Dunia kwa kichapo cha mabao 4-3 kwa njia ya matuta

Wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia Urusi wameyaaga rasmi mashindano hayo kwa kichapo cha mabao 4-3 kwa njia ya matuta dhidi ya Croatia.

Mchezo huo ulifikia hatua hiyo baada ya dakika 120 kwenda sare ya mabao 2-2 na changamoto ya mikwaju ya penati ikaamuliwa kupigwa.

Mabao ya yaliyopatikana ndani ya dakika 90 kwa upande wa Urusi yaliwekwa kimiani na Denis pamoja na Fernandez.

Wakati huo Croatia walijipatia mabao yao kupitia kwa Andrej na Vida.

Baada ya michezo hatua ya robo fainali kukamilika jana, Croatia walioingia nusu fainali watacheza dhidi ya England huku Ufaransa wakikipiga na Ubelgiji.

No comments:

Post a Comment