Saturday, 14 July 2018

WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imelipa sh. bilioni 43 zikiwa ni madeni kwa watumishi wa umma na kati ya hizo sh. bilioni 16.25 zimelipwa kwa walimu.

“Hadi kufikia mwisho wa mwezi uliopita, jumla ya sh. bilioni 43 zimelipwa kwa watumishi 27,389 ambao kati yao watumishi 15,919 ni wa sekta ya elimu tu na madeni yao yanafikia sh. bilioni 16.25,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Julai 13, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga akiwa aktika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

“Mapema mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli aliahidi kutoa sh. bilioni 200 za kulipa madeni ya watumishi na hadi sasa madeni ambayo yameshahakikiwa ni sh. bilioni 127 na mengine ni ya wazabuni,” amesema. 

Amesema hivi sasa Serikali inadhibiti uzalishaji wa madeni ya watumishi kwa kuzuia uhamisho kama hakuna fedha, kuzuia rufaa zisizokuwa za lazima na ambazo hazina ufuatiliaji wa waganga wakuu wa mikoa na wilaya, na kuhimiza matumizi ya Bima ya Afya kwa watumishi wa umma.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Julai 13, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack . 
 Baadhi ya Watumishi na Viongozi wa vyama vya Siasa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Julai 13, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Julai 13, 2018. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI,  Joseph Kakunda na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment