Wednesday, 25 July 2018

Waziri Mkuu aungana na Wakazi wa Wilaya ya Kinondoni kufanya usafi Coco Beach


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo ameungana na wakazi wa wilaya ya Kinondoni kufanya usafi katika eneo la ufukwe wa Coco Jijini Dar es Salaam na kutoa wito kwa manispaa hiyo kuboresha maeneo ya kutolea huduma ili yaendane na hadhi ya fukwe hiyo.

Akizungumza mara baada ya kufanya usafi na kupanda mti katika eneo hilo waziri Mkuu ameitaka halmashauri ya manispaa ya Kinondoni kuhakikisha wanaboresha vibanda vya watoa huduma za vyakula, ulinzi na mandhari ya eneo hilo ili liwe kivutio zaidi kwa wananchi wanaolutumia.

Majaliwa ambaye ameambatana na Mke wake Mama Marry Majaliwa akaelezea maamuzi yaliyofikiwa kuhusiana na fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya mashujaa hapa nchini.

Awali akimkaribisha waziri Mkuu, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Happi ameelezea mipango mbalimbali ya kuboresha ufukwe wa Coco na kuahidi kusimamia usafi katika eneo hilo.

Tanzania huadhimisha siku ya mashujaa wake waliopoteza maisha katika harakati za kuipigania nchi ifikapo Julai 25 ya kila mwaka.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: