Wednesday, 25 July 2018

Washiriki Miss Kanda ya Kaskazini wahimizwa kuhamasisha Utalii Nchini


Na Ferdinand Shayo, Arusha
Warembo wanaoshiriki shindano la Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini wametakiwa kuhamasisha Jamii ya Watanzania na watalii kutoka nje ya nchi kutembelea vivutio vya utalii wa utamaduni vilivyoko jijini Arusha ikiwemo Makumbusho ya Africa Culture heritage.

Mkurugenzi wa kituo cha makumbusho ya africa Culture Heritage cha jijini Arusha  Saifuddin Khanbhai amewataka warembo wanaowashiriki katika shindano ya Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini kuhimiza Utalii wa utamaduni haswa kwa watalii wa ndani ili kuendeleza Tamaduni zilizohifadhiwa katika makumbusho mbalimbali.

Akizungumza na wanyange hao mara  baada ya kutembelea kituo hicho Seif Amesema mwitikio wa watanzania ni mdogo sana wanaotembelea kitu hicho huku akiwaomba kutumia fursa walionayo katika jamii kuhamsisha italii wa ndani kwani utawafanya watanzania wengi kujua historia ya nchi.

Ameendelea kusema  kama watanzania wataweka tamaduni wamutembelea vituo mbalimbali vya makumbusho kutasaidia kuwajengea uzalendo na kuongeza juhudi katika uwajibikaji hali ambayo atasaidia kukuza pato la taifa.

Kwa upande mkurugenzi wa Kismaty Advert Media  ambao ndio waandaji wa shindano hilo kwa kanda ya kaskazini anasema maandalizi ya shindano yako katika hatua za mwisho katika kuelekea kilele cha shindano hilo julai 28 katika ukumbi wa naura Springs uliopo katika jiji la arusha.

Huku akisema lengo la kuwapeleka wanyange  hao katika makumbusho hayo  Culture Hertage ni kuzid kuhamasisha jamii kutembelea makumbusho mbalimbali kwani zipo kwa ajili ya watanzaia pia na sio watu kutoka mataifa ya nnje pekee.

Huku baadhi ya washiriki washindano hilo wakionesha furaha yao baada ya kuona historia mbalimbali za makabila yaliopo mchini pamoja na michoro.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: