Tuesday, 17 July 2018

Wanawake wazuia Wanaume kuzika mwenzao Mto wa Mbu


Taarifa kutoka katika kata ya mto wa Mbu, Arusha ni hii ya wanawake kukataa wanaume wasishiriki kwenye mazishi ya mama anayejulikana kwa jina la Ruth kutokana nakudaiwa kuuawa kisha kubakwa na watu wasiojulikana huku wakiwatuhumu wanaume wa eneo hilo kuhusika na matukio hayo.

Wakati jeshi la polisi Arusha likithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mbunge wa jimbo hilo la Monduli Julius Kalanga amesema wanawake hao wamefikia uamuzi huo baada ya matukio hayo kukithiri huku akilitaka jeshi la polisi kuchunguza na kuchukua hatua.

“Pamoja na kuwa ni mtu wa nane kuuawa wanawake wameonyesha hisia zao kwa kudhani kwamba wanaume ndio wanaowauwa kwani tangu matukio haya yatokee haijawahi kutokea mtu aliyehukumiwa kutokana na matukio haya” -Mbunge Kalanga

No comments:

Post a Comment