Sunday, 8 July 2018

Walimu watakiwa kuwa makini wanapowasilisha madai yao


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amewataka walimu nchini kuzingatia taratibu za kuwasilisha madai yao serikalini kutokana na madai mengi ya walimu yanayowasilishwa kuwa na kasoro na mengine kutokuwa na vithibitisho vya uhalali hali inayosababisha kuchelewa kulipwa.

Profesa Ndalichako ameyasema hayo wakati akizungumza na walimu wilayani Kasulu, ambapo amesema serikali inaendelea kulipa madai ya walimu nchini lakini ni muhimu walimu kutimiza wajibu wao na halmashauri kushirikiana na chama cha walimu kumaliza matatizo ya walimu katika halmashauri.

Kwa upande wao viongozi wa chama cha walimu CWT wilayani Kasulu, wameitaka serikali kuongeza kasi ya kulipa madai ya walimu pamoja na kuboresha vitendea kazi ili kurahisisha kazi ya kufundisha na hivyo kuongeza ufaulu.

No comments:

Post a Comment