Na manuel kaminyoge, mkoani songwe,

Afisa tarafa ya vwawa wilayani Mbozi mkoani Songwe Haji  Hamisi Ibrahimu ameamuru waliokuwa viongozi kijiji cha mbimba akiwemo mtendaji wa kijiji , mwenyekiti wa kijiji, pamoja na watia sahihi kwenye akaunti ya kijiji hicho kuwekwa chini ya ulinzi na hatimaye wakabiziwe mikononi mwa polisi baada ya kubainika wameiba fedha kwenye akaunti ya kijiji   zaidi ya sh. Milioni tatu.

 Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi za kijiji hicho Haji  amesema kuwa japo watu hao wamestaafu uongozi lazima watafutwe popote walipo na sheria ichukue mkondo wake huku akitoa wito kwa viongzi wengine kuacha kutumia fedha za wananchi bila idhini ya wanakijiji.

Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho menisoni kamwela ameshukuru kwa hatua zilizochukuliwa na tarafa huyo ambapo amesema kuwa fedha hizo zilibwa kwenye akaunti ya kijiji toka mwaka 2012 huku akitoa wito kwa viongozi wa ngazi za juu  kuchukua hatua pale inapo bainika kuwa kuna ubadhilifu wa fedha za uma kitendo ambacho kina kwamisha maendeleo .

Aidha bosko njante (mwananchi)amesema kuwa serikali ya awamu ya tano sio ya mchezo mchezo na ina wahitaji viongozi wenye uwezo wa kuchukua hatua ambapo amempongeza afisa tarafa kwa jithada anazozifanya za kuhakikisha maendeleo kwa wananchi yanapatikana.

“raisi magufuli anahitaji viongozi kawa nyinyi mnaotetea wananchi wanyonge na wa hali ya chini “amesema bosko
Share To:

msumbanews

Post A Comment: