MAMLAKA ya Elimu ya Ufundi (VETA) katika chuo chake cha Kipawa Dar es Salaam, imevumbua mfumo kwa waendeshaji bodaboda kulazimika kuvaa kofi a unaofanya bila kuvaa kofi a pikipiki isiwake.

Kutokana na uvumbuzi huo, imeomba serikali katika kukabiliana na athari vichwani kwa waendesha bodaboda, kuweka sheria ya pikipiki zote kwenda VETA kufungiwa mfumo huo kabla ya kuendelea na matumizi kama walivyofanya kwa sare za madereva. 

Pikipiki hiyo iliyopo katika viwanja ya Maonesho ya 42 ya Biashara, imewekwa kifaa maalumu na kwenye kofia za pikipiki ‘helmet’ ambayo ndiyo inaendesha mfumo mzima.

Akizungumzia mfumo huo, mwanafunzi Rentius Pesha alisema kofia hizo ni kwa dereva wa bodaboda pamoja na abiria wake, na lazima kofia iwekwe kichwani ili iwake na siyo sehemu nyingine. 

Alisema lengo la kubuni mfumo huo ni kubainisha teknolojia siyo lazima itoke nje ya nchi, bali mamlaka hiyo ina uwezo wa kuvumbua teknolojia mbalimbali ikiwemo kusaidia kuokoa nguvukazi ya taifa kwa kuanzia na kuokoa wanaopata matatizo vichwani. 

Mwalimu katika chuo hicho cha Kipawa, Anneth Mganga aliomba serikali kutunga sheria katika kutumia mfumo huo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: