Saturday, 7 July 2018

UWT yatakiwa kuachana na siasa za kukashifiana


Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera,Bunge, Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde amelitaka baraza la umoja wa wanawake wa CCM kuunda kampuni na vikundi vitakavyosajiliwa ili kuweza kupata fursa ya fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali badala la kusubiri fedha za chama.

Akizungumza na baraza la UWT Dodoma mjini, Mavunde ameitaka UWT kuachana na siasa za zamani za kukashifiana na kutukanana na kujielekeza kwenye siasa za sasa za kushawishi watu kwa kujiletea maendeleo kupitia fursa mbalimbali zinazojitokeza katika miradi ya serikali.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Dodoma mjini, Robert Mwinje amesema amewaasa kama wanajiona hawatoshi kugombea nafasi mbalimbali katika chaguzi zijazo washawishi watu wenye uwezo  kugombea nafasi hizo na wakichagua wagombea wabovu  CCM itapata wakati mgumu kwa kuwa lengo la chama cha mapinduzi ni kushinda uchaguzi na kuendelea kushika dola.

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dodoma Neema Majule amesema lengo la UWT mkoa ni kuhakikisha linaunganisha kupitia mshikamano na umoja na kuifanya kuwa kimbilio la wanawake wa ngazi zote na hasa wenye lengo la kujikomboa kiuchumi kipitia miradi mbalimbali ya maendeleo.

No comments:

Post a Comment