Wanananchi wa Nyamagana  Kata ya Kishiri wametoa shangwe na nderemo katika Mkutano wa hadhara wa Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula na wananchi alipo kuwa akitoa mrejesho wa urasimaji wa maeneo ya makazi kwa  upimaji shirikishi. Mhe Mabula amesema wamekuwa na Vikao na halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa siku tatu mfululizo na wote kwa pamoja wamekubaliana  urasimishaji wa maeneo uhusishe upimaji Shirikishi.

Mhe Mabula ameipongeza serikali ya awamu ya tano inayoogozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makadhi kuwajari wananchi wanyonge kupitia Upimaji Shirikishi.  Amefafanua kuwa serikali kupitia halmashauri ya Jiji la Mwanza imekusudia kuboresha mipango miji  kupiti Idara Ardhi pamoja na Mipango miji kwa kukubali  Mitaa  mitano kata ya Kishiri ikiwa Mtaa wa Kanindo, Kishiri B, Kaneno, Abukaga pamoja na Fugamila Mashariki  kunufaika na upimaji shirikishi kwa gharama ya shilingi 200,000 kwa kila kiwanja kwa mujibu wa taratibu. Hii ni kukabiliana na changamoto iliyojitokeza kwa wananchi kujenga makazi ya kudumu kwa kutokufuata mchoro wa mwaka 2012.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: