Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Kanda ya Ziwa imekamata shehena ya malighafi ya mafuta ya kupikia aina ya Poa Cooking, yanayodaiwa kutengenezwa na viambata vya sumu katika kiwanda cha kuchambua pamba na kusindika mafuta cha ICK cha jijini Mwanza.

Inadaiwa mmiliki wa bidhaa hizo, Mfanyabiashara Mtanzania mwenye asili ya Asia, Baweshi Gandecha, alikuwa anauza tofauti na masharti ya uagizaji wake hivyo kutishia usalama wa walaji.

Meneja wa TFDA Kanda ya Ziwa, Moses Mbambe, amesema bidhaa hizo zina madhara makubwa kwenye mfumo wa chakula kwani husababisha matobo kutokana na kuwa na tabia ya kuunguza chakula na mdomo.

“Mafuta haya yana madhara ya kiafya kwa watumiaji kutokana na kutengenezwa kwa kutumia kemikali aina ya ‘Caustic Soda’ ambayo huathiri mfumo wa chakula kwa kuunguza mfumo huo na midomo na kusababisha matokeo kwenye mfumo wa chakula,” amesema.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: