Friday, 27 July 2018

Tanzia: Eric Shigongo afiwa na Mmama yake mzazi


Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Group, Eric James Shigongo usiku wa kuamkia leo amepatwa na msiba mzito wa kuondokewa na mama yake mzazi Bi. Asteria Kapera.

Bi. Kapera amefariki dunia alfajiri ya leo Julai 27, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu taarifa iliyotolewa na Meneja Mkuu wa Global Publishers Abdallah Mrisho amesema kuwa msiba utakuwa nyumbani kwa marehemu maeneo ya Mikocheni B jijini Dar es Salaam ambako taratibu zote za msiba zitafanyika
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: