Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo ametangaza ajira za Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari zipatazo 4840 ikiwa ni sehemu ya kibali cha ajira cha kuajiri walimu 6840.

Akitangaza ajira hizo katika Ofisi Ndogo za Wizara zilizopo Magogoni Dar es salaam Mhe. Jafo alisema katika kibali hicho kilichotoka Mei 30,2018 kilitoa nafasi ya kuajiri walimu 4785 wa Shule za Msingi, 55 Mahitaji Maalumu na  2000 ni Walimu wa Sekondari wanaofundisha masomo ya sayansi kwenye shule za Sekondari ambao mchakato wake bado unaendelea.

Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari Mhe. Jafo amesema kuwa “Walimu tunaotangaza vituo vyao vya kazi leo ni wale waliotuma maombi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mwezi Dec 2017 na Walimu 2767 walipangiwa vituo vya kazi mwezi Januari 2018 na hawa tunaotangaza leo ni miongoni mwa walimu wenye sifa waliokosa nafasi kwa kipindi hicho cha mwaka 2017”.

Pia amewataka walimu wote waliopata nafasi kuripoti katika vituo vyao vya kazi kuanzia tarehe 23 Julai, 2018 hadi tarehe 7 Agosti 2018  wakiwa na vyeti halisi vya Taalumu vya Kidato cha Nne/Sita, vyeti halisi vya mafunzo ya ualimu katika ngazi husika pamoja na  cheti halisi cha kuzaliwa.

Aidha Waziri Jafo ametoa maelekezo Maalumu kwa Walimu wote waliopangiwa vituo vya kazi kuwa Vituo vya kazi vya walimu hao ni katika shule za msingi na sekondari na sio Makao Makuu ya Halmashauri na mwajiriwa yeyote atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu kisha akaondoka katika kituo chake cha kazi alichopangiwa Serikali itamchukuliwa hatua kali kwa mujibu wa Sheria.

Alisisitiza kuwa hakuna mwalimu atakayekubadiliwa kubadilishiwa kituo kwa sababu yeyote ile na kila mwajiriwa aatakayeshindwa kuripoti katika kituo chake kwa muda uliopangwa nafasi zao zitachukuliwa na Walimu wengine 5,220 wenye sifa ambao bado bado wamekosa nafasi za ajira katika awamu hii.

Orodha ya majina ya Walimu waliopangiwa katika Vituo vya Kazi kwenye Shule za Msingi na Sekondari yanapatika kwenye Tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI www.tamisemi.go.tz.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: