Sunday, 8 July 2018

Singida United yafunguka sababu zilizopelekea kumsajili Kipa wa Njombe


Uongozi wa Singida United umefunguka na kueleza sababu zilizopelekea wakamsajili aliyekuwa kipa wa Njombe Mji, David Kisu.

Kwa mujibu wa Mkurungenzi wa Singida United, Festo Sanga, ameanika sababu na kusema alikuwa ni kipa bora uwanjani licha ya kuwa timu yake imeshashuka daraja.

Sanga amesema licha ya ubora wake, amemueleza Kisu kama mchezaji aliyekuwa na msaada mkubwa wakati akiwa Njombe Mji ikiwa ni moja ya kigezo kikubwa kwao kilichopelekea wakamsajili.

Kisu ambaye alikuwa akiichezea Majimaji FC katika msimu wa 2017/18, amemalizana na mabosi wa Singida kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu.

Licha ya kuichezea Njombe Mji, Kisu aliwahi pia kuichezea klabu ya Simba akiwa kama kipa wa akiba miaka kadhaa iliyopita.

No comments:

Post a Comment